IQNA

Watu milioni 2 kushiriki katika kipindi cha Qur'ani Iran

12:52 - June 28, 2011
Habari ID: 2145677
Mkurugenzi wa Radio ya Qur'ani katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa kipindi cha "Qur'ani, Kitabu cha Mwamko" kinatazamiwa kuwavutia karibu washiriki milioni mbili nchini.
Ahmad Layali amesema, 'kutokana na uzoefu wa mwaka jana, inatabiriwa kuwa mwaka huu watu milioni 2 watashiriki katika kipindi hiki'.
Ameongeza kuwa baadhi ya mashirika ya mawasiliano ya simu za mkono yamependekeza kutuma masuala ya kipindi kwa wenye simu za mkono. 'Iwapo hilo litaafikiwa basi idadi ya washiriki inaweza kufika milioni tano', amesema.
Kuhusu sherehe za kufunga kipindi hicho, Layali amesema: "Sherehe kubwa zitafanyika sambamba na kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Hassan (AS)".
813395
captcha