Mkurugenzi wa Jumba la Makumbusho la Imam Hussein Alaa Ahmad Dhiyauddin amesema kuwa jumba hilo ni sehemu ta "Tamasha ya Saba ya Kimataifa ya Msimu wa Machipuo wa Shahada" ambayo itasimamiwa na Haram ya Imam Hussein (as) na Hadhrat Abbas (as) kuanzia tarehe 4 hadi 9 Julai.
Alaa Ahmad Dhiyauddin ameongeza kuwa wahadhiri wa vyuo vikuu na wataalamu wa masuala ya majumba ya makumbusho watahudhuria sherehe za ufunguzi.
Mkurugenzi wa majumba ya makumbusho ya Iraq Amira Eidan al Dhahab pia amezungumzia sifa za kipekee za jumba hilo la makumbusho nchini Iraq.
Kamati inayosimamia Tamasha ya Kimataifa ya Msimu wa Machipuo wa Shahada tayari imeanza maandalizi ya tukio hilo la kimataifa na inashughulikia masuala ya jinsi ya kutoa huduma kwa wageni na watalii wataoshiriki katika tamasha hiyo.
Shakhsia mbalimbali wa kidini, kielimu ma wanafasihi kutoka nchi mbalimbali za Kiarabu na zisizokuwa za Kiarabu wamealikwa kushiriki katika tamasha hiyo. 816597