IQNA

Kikao cha Jumuiya ya Nchi za Kiislamu chaanza leo Astana

23:05 - June 28, 2011
Habari ID: 2146130
Rais Nursultan Nazarbayev wa Kazakhstan mwenyeji wa mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Kiislamu ametangaza leo kwamba Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC imebadilishwa jina na kuwa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (Organization of The Islamic Cooperation (OIC)).
Nazarbayev amesema katika ufunguzi wa mkutano huo kwamba nchi wanachama wa OIC zinamiliki asilimia 90 ya vyanzo vya maliasili duniani lakini zina hisa ndogo sana ya pato la taifa. Amesema nchi za Kiislamu zina uwezo na utajiri mkubwa na kwa msingi huo zinapaswa kupanua zaidi ushirikiano wao. Ametoa pendekezo la kuundwa Baraza la Mazungumzo ya Kiuchumi katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na amezishauri nchi wanachama kuchukua uamuzi juu ya suala la kuanzisha mfumo wa kusaidiana katika masuala ya kudhamini chakula. Rais wa Kazakhstan amepinga madai ya nchi za Magharibi ya kuuhusiaha Uislamu na ugaidi na ametoa pendekezo la kuanzishwa chombo cha habari cha nchi zote za Kiislamu kwa ajili ya kuarifisha dini ya Kiislamu kote duniani. 816591




captcha