Ripoti ya Nne ya OIC kuhusu chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia kuanzia Mei 2010 hadi Aprili 2011 imetangazwa katika Kikao cha 38 cha Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa OIC huko Astana Kazakhstan.
Ripoti hiyo imesema chuki dhidi ya Uislamu ni mwenendo unaotia hofu na unaohatarisha amani na usalama wa dunia. Ripoti hiyo ina juzuu sita ambazo zinafafanua kuhusu aina mbalimbali za chuki dhidi ya Uislamu. Ripoti hiyo imeonya kuhusu kuendelea kampeni za kisiasa dhidi ya Waislamu katika baadhi ya nchi za Ulaya na Marekani. Imesema chuki dhidi ya Uislamu sasa imechukua sura rasmi katika baadhi ya nchi.
Ripoti hiyo ya OIC pia imetoa mapendekezo ya kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu na kusisitiza juu ya udharura wa kufanyika juhudi za kimataifa kukabiliana na suala hilo.
817399