IQNA

Wiki ya Kuhifadhi Qur'ani kufanyika Thailand

14:30 - June 29, 2011
Habari ID: 2146605
Wiki ya Tamasha ya Kuhifadhi na Kusoma Qur'ani itaanza tarehe 4 hadi 8 Julai katika mji wa Jala nchini Thailand.
Kituo cha habari cha ISESCO kimeripoti kuwa wiki hiyo ya mafunzo na elimu itasimamiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ISESCO kwa ushirikiano wa Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia na Chuo Kikuu cha Jala.
Lengo la wiki hiyo ya Qur'ani ni kuwahamasisha wanafunzi na vijana wa Kiislamu wa eneo hilo la Jala kuhifadhi na kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu, kutathmini mahitaji ya Waislamu wa eneo hilo katika nyanja za mafunzo ya Qur'ani kwa watoto wadogo na kusaidia juhudi za kulinda turathi za Kiislamu nchini Thailand.
Wiki hiyo ya Qur'ani itakuwa na vikao vya kuchunguza njia za kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu kwa wasiokuwa Waarabu, vikao vya darsa za walimu mashuhuri wa Qur'ani na masomo ya walimu wa Qur'ani.
Shughuli za wiki hiyo zitasimamiwa na Abdul Ilah Bin Arafa mtaalamu wa turathi za kiutamaduni wa ISESCO na Abdulaziz al Iyadi ambaye ni mwalimu wa sayansi ya Qur'ani Tukufu kutoka Morocco. 817404

captcha