Rais Mahmoud Ahmadinejad amesema hayo katika sherehe za ufunguzi wa Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayofanyika hapa mjini Tehran.
Mashindano hayo yanawashirikisha mahufadh 45 na maqarii 57 kutoka zaidi ya nchi 60 duniani.
Rais Ahmadinejad ameongeza kuwa, Qur'ani ni taa ya uongofu na ni nuru isiyozima.
Vile vile amesema, Qur'ani Tukufu ni njia iliyonyooka na ndiyo siri ya mafanikio na wokovu wa mwanaadamu.
Akiendelea na hotuba yake kwenye sherehe hizo za ufunguzi wa Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu, Rais Ahmadinejad ameongeza kuwa, Qur'ani ni kitabu cha uhai na utawala wa sheria za Mwenyezi Mungu na kwamba kama tunataka tuyashinde matatizo yote yanayoikabili jamii ya mwanaadamu duniani leo, basi hatuna budi kutekeleza kikamilifu mafundisho ya Mwenyezi Mungu yaliyomo kwenye Qur'ani Tukufu. 817731