Sherehe za ufunguzi zimehudhuriwa na mkuu wa Idara ya Utamaduni ya Iran Mahdi Gholi Rokni na Balozi wa Iran nchini Sri Lanka Rahimi Gorji pamoja na wanazuoni wa Kiislamu nchini humo.
Kituo hicho ambacho kimefunguliwa baada ya kupata idhini ya Idara ya Masuala ya Waislamu nchini Sri Lanka kitakuwa na shughuli kadhaa zikiwemo za kiraa na kuhifadhi Qur’ani Tukufu. Kituo hicho pia kitaandaa mashindano ya Qur’ani.
Mkuu wa Idara ya Utamaduni ya Iran nchini Sri Lanka amesema kuna mpango wa kuanzisha Darul Qur’ani katika mji wenye Waislamu wengi wa Valechina.
818028