IQNA

Makarii wa Qur’ani hutamani kushiriki mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Iran

17:06 - July 02, 2011
Habari ID: 2147190
Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Iran hufanyika kwa kiwango cha juu na hivyo kila karii na hafidh wa Qur'ani duniani hutamani kushiriki katika mashindano hayo.
Hayo ni kwa mujibu wa karii wa Misri Muhammad Ali Tarouti ambaye amesema pia kuwa jopo la majaji katika mashindano ya Iran huwajumuisha wataalamu bingwa wa Qur’ani duniani.
Akizungumza na IQNA katika ukumbi wa mashindano ya Qur’ani mjini Tehrani, Tarouti amesema mashindano ya mwaka huu ni ya kiwango cha juu.
Muhammad Ali Tarouti ambaye ni kaka yake karii mashuhuri wa Misri Abdul Fattah Tarouti ameongeza kuwa ana furaha kuhudhuria mashindano ya Tehran na kusikiliza kiraa za kuvutia na vilevile kujuana na makarii na mahafidh kutoka nchi mbalimbali duniani.
Karii huyo kutoka Misri amewapongeza viongozi wa Iran kwa juhudi zao katika uga wa Qur’ani. ‘Sijaona rais yeyote duniani anayewapenda na kuwaheshimu makarii wa Qur’ani kama Rais wa Iran. Kwa niaba ya makarii wote wa Qur’ani Tukufu nchini Misri, nawashukuru waandalizi na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran’, amesema Tarouti. 817963
captcha