IQNA

OIC yataka kutambuliwa rasmi nchi ya Palestina

20:27 - July 02, 2011
Habari ID: 2147690
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu Ekmeleddin Ihsanoglu ameutaka Umoja wa Mataifa utambue rasmi nchi huru ya Palestina.
Ihsanoglu amewaambia waandishi wa habari baada ya kumalizika mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Kiislamu nchini Kazakhstan kwamba nchi zote zilizoshiriki katika mkutano huo zimesisitiza kwamba ardhi zote zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni zinapaswa kukurejeshwa kwa wananchi wa Palestina na Quds itambuliwe kuwa ni mji mkuu wa Palestina.
Ihsanoglu ameongeza kuwa mkutano wa OIC mjini Astana pia ulijadili masuala yanayohusiana na uwezo na ustahiki wa Palestina wa kuwa mwanachama katika Umoja wa Mataifa.
Viongozi wa Palestina wanakusudia kuwasilisha ombi la kutambuliwa rasmi nchi huru ya Palestina katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu. 818298


captcha