IQNA

Chapa mpya ya msahafu wa kitaifa yazinduliwa Qatar

18:54 - July 03, 2011
Habari ID: 2148288
Chapa mpya ya msahafu wa kitaifa wa Qatar ambao umefanyiwa mabadiliko katika kusarasa zake imezinduliwa mjini Doha kwa hima ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya nchi hiyo.
Nakala mpya ya msahafu wa kitaifa wa Qatar imechapishwa na kiwanda cha uchapishaji cha Mas nchini Uturuki na zimetumika karatasi zenye ubora wa hali ya juu kiasi kwamba kila karatasi moja ina uzito wa gramu 36.
Wazara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar imezindua baadhi ya nakala za msahafu huo wa kitaifa katika sherehe iliyofanyika kwenye Hoteli ya Sheraton mjini Doha katika hadhara ya watoto 63 kutoka nchi 16 za Kiarabu na Kiislamu.
Nakala mpya ya masahafu wa kitaifa wa Qatar ina karatasi zenye ubora wa juu na upana wake bila ya kujumuisha jalada lake ni milimita 12.
Miongoni mwa sifa za msahafu huo ni uangalifu mkubwa wa kuchapishwa kwake, rangi zake zinazoonekana vyema na mapambo yaliyotumiwa kuremba kandokando ya aya za Qur'ani. 819149
captcha