IQNA

Msafara wa Uhuru – 2 kuelekea Gaza leo

10:29 - July 04, 2011
Habari ID: 2148549
Msafara wa meli za misaada ya kibinadamu wa Uhuru-2 ambao juzi ulizuiwa na serikali ya Ugiriki kuelekeza Ukanda wa Gaza huko Palestina unaanza leo safari ya kuelekea katika eneo hilo.
Shirika la Habari la Kuwait (KUNA) limeripoti kuwa meli za msafara huo zitaanza leo safari ya kuelekea Gaza licha ya kuzuiwa na serikali ya Ugiriki.
Timu ya Ulaya inayofanya jitihada za kuvunja mzingiro wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Ukanda wa Gaza ilitangaza jana kuwa meli kadhaa za Msafara wa Uhuru-2 zitaelekea Gaza hii leo. Timu hiyo imesema juhudi zinafanyika kujaribu kuishawishi serikali ya Ugiriki ibatilishe uamuzi wake wa kuzuia meli za msafara huo kutumia bandari zake kwa ajili ya kuelekea Gaza.
Imesema kuwa amri ya serikali ya Ugiriki ya kuzuia msafara huo haikutolewa na mahakama ya nchi hiyo na kwamba hiyo ni hatua isiyokuwa na kibinadamu.
Imeongeza kuwa msafara huo wa Uhuru-2 sasa una meli 9 baada ya kundi moja la watu wasiojulikana ambao inaaminika kuwa wanashirikiana na shirika la ujasusi la Israel Mossad kuharibu moja ya meli za msafara huo. 819315


captcha