Kituo cha habari cha iccdny kimeripoti kuwa semira hiyo itachunguza njia za kuzama na kudurusu Qur'ani kwa kina, maudhui zilizozungumzwa katika juzuu mbalimbali za Qur'ani na muujiza wa kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Kituo cha Kiislamu cha New York pia kitakuwa na mashindano ya Qur'ani Tukufu katika mwezi wa Ramadhani ambayo yatawashirikisha watoto wenye umri wa chini ya miaka kumi katika hifdhi ya sura ya Nuh na vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 watakaoshindana katika kuhifadhi sura ya Dukhan. 819249