IQNA

OIC yatakiwa kuandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani

17:33 - July 04, 2011
Habari ID: 2148815
Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu OIC limetakiwa kuandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani.
Wito huo umetolewa na Mohammad Ihasan Sayyid Hassan ambaye ni jaji kaitka Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran yanayofanyika kati ya 27 Rajab na 2 Shaaban.
Amesema kuwa OIC ni taasisi muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu na hivyo inapaswa kuongoza harakati za Qur'ani duniani.
Mohammad Ihasan Sayyid Hassan ameishikuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuwaalika Waislamu kutoka nchi za Kiislamu na zisizo kuwa za Kiislamu kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Tehran. Ameongeza kuwa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Tehran ni nembo ya umoja wa Waislamu duniani.
819710
captcha