Kwa mujibu wa tovuti ya al Shahda, Sheikh al Azhar ameongeza kuwa: 'Mimi niko tayari kuenda Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ninajitahidi kuwakurubisha wanazuoni wa Al Azhar na Marajii wa Kishia nchini Iran'.
Sheikh Ahmad Tayyib amesema kuwa Al Azhar ni nyumba ya Waislamu na milango yake iko wazo kwa makundi na madhehebu mbalimbali za Kiislamu. Amesisitiza kuwa 'Waislamu wa madhehebu ya Shia ni sehemu isiyotenganika ya umma wa Kiislamu na sisi tunaswali nyuma ya maimamu wa Kishia. ameongeza kuwa madai kwamba Mashia wana Qur'ani nyingine tofauti na hii iliyoko ni uongo mtupu'.
Sheikh Ahmad Tayyib amekumbusha kuwa, 'hakuna hitilafu kati ya Mashia na Masuni na tafauti zilizopo baina ya wafuasi wa madhehebu hizo zinarejea katika masuala ya Uimamu'.
Duru kutoka Al Azhar zinaarifu kuwa Sheikh Tayyib amechukua uamuzi wa kukurubisha Masuni na Mashia na moja ya hatua zinazochukuliwa katika uwanja huo ni kufungua milango ya Al Azhar kwa wanafunzi wa Kishia na kuwarushusu wanazuoni wa ngazi za juu wa Kishia (Marajii) kuwa wanachama wa Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya Al Azhar.
819887