IQNA

Matokeo ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Tehran

15:33 - July 05, 2011
Habari ID: 2149165
Wawakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika vitengo vya hifdhi ya tajwidi wamechukua nafasi za kwanza katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu yaliyowashirikisha watu 96 kutoka nchini 61 duniani.
Mshiriki kutoka Tanzania Ibrahim Ramadhan Shaaban ametokea wa tano katika hifdhi. Jopo la majaji wa mashindano hayo jana usiku lilimtangaza Abbas Hashemi kutoka Iran kuwa mshindi wa kwanza katika usomaji wa tajwidi akifuatiwa na Suhaybuddin kutoka Indonesia, Ahmad bin Yusuf kutoka Bangladesh, Muhammad at Tarouti kutoka Misri na Sayyid Thamaruddin Samadev kutoka Tajikistan. Jopo hilo limetangaza pia kuwa, Murtadha Muhammadnejad kutoka Iran ameshika nafasi ya kwanza katika hifdhi akifuatiwa na Miqdad Mudhafar Jasim na Farhad Yunus Hasan kutoka Iraq, Kassim Sukuna kutoka Mali na Ibrahim Ramadhan Shaaban kutoka Tanzania.
Katika kitengo cha utafiti wa Qur’ani pia, Mahdi Akbarnejad kutoka Iran amechukua nafasi ya kwanza. Leo Jumanne, washiriki na waandaaji wa mashindano hayo ya 28 ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu wanatarajiwa kuonana na Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Washindi wa kwanza hadi wa tano wamepewa zawadi maalumu kwenye mashindano hayo.
820122
captcha