Hayo yamesemwa na karii na mwakilishi wa Uturuki katika kitengo cha kiraa cha Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran Fatih Qalic Oglu. Ameiambia IQNA kwamba mashindano ya Qur'ani nchini Iran yanafanyika katika vitengo kadhaa na kwamba kamati ya majaji wa mashindano hayo imefanya kazi zake kwa makini na ushirikiano mkubwa.
Fatih Qalic amesema sheria zinazotumiwa na majaji wa mashindano ya Qur'ani zinafanana na ndizo zilizotumiwa katika mashindano ya sasa ya Tehran.
Amesema kiwango cha Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani mjini Tehran ni cha juu na kuongeza kuwa kuwepo makarii na mahafidhi kutoka nchi mbalimbali za dunia katika mashindano haya kumeyapa sifa makhsusi. Amesisitiza kuwa amepata uzoefu mkubwa kutokana na kushiriki kwake katika tukio hilo la kimataifa ambalo amesisitiza kuwa hatalisahau.
Msomaji huyo wa Qur'ani kutoka Uturuki amesema kufanyika mashindano ya kimataifa ya Qur'ami mara 28 nchini Iran ni kielelezo cha jinsi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inavyojishughulisha sana na masuala ya Qur'ani.
Qalic Oglu amesema wasomaji Wairani katika mashindano haya ya kimataifa wamethibitisha uwezo wao mkubwa licha ya kuchuana na wasomaji wenye uwezo mkubwa kutoka nchi za Ujerumani, Thailand na Ufilipino. 820565