IQNA

Mafunzo ya muda ya Qur'ani yaanza Sudan

22:58 - July 05, 2011
Habari ID: 2149643
Mafundisho ya muda ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yalianza jana nchini Sudan yakisimamiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ISESCO.
Mafunzo hayo ya ISESCO na Taasisi ya Ulinganiaji wa Kiislamu ya Sudan yatafanyika katika maeneo mbalimbali ya jiji la Khartoum.
Lengo la mafunzo hayo limetajwa kuwa ni kustawisha utamaduni wa kuhifadhi Qur'ani kati ya vijana wa Kiislamu na kutayarisha uwanja mzuri wa kupanua zaidi shule za Qur'ani.
Katika mafunzo hayo wataalamu wa hifdhi ya Qur'ani watafundisha mbinu za kisasa za kutoa mafunzo. 820313
captcha