Hayo yamesemwa na Azhar bin Othman bin Abdullah, jaji wa Malaysia katika mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran yaliyomalizika siku chache zilizopita. Amesema kuwa amekwishashiriki mara mbili katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Saudi Arabia na anashiriki kila mwaka katika Mashindano ya Kimataifa ya Malaysia kama jaji na mwamuzi lakini kwa maoni yangu Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran ndiyo yanayopokewa mno na wasomaji na mahafidhi wa kimataifa.
Ameongeza kuwa mwaka jana wasomaji Qur'ani kutoka nchi 55 walishiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia lakini mashindano ya mwaka huu ya Tehran yamewashiriki makarii kutoka zaidi ya nchi 60 duniani.
Jaji huyo wa Qur'ani wa kimataifa wa Malaysia amesema: "Nimeshiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Malaysia na Saudi Arabia kama jaji na mwamuzi lakini mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran ni ya kiwango cha juu zaidi ikilinganishwa na mashindano hayo.
Bin Abdullah amesema makarii, mahafidhi, walimu na majaji mashuhuri wa ulimwengu wa Kiislamu wana hamu kubwa ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran ni ndiyo maana tunaona idadi kubwa ya washiriki kutoka pembe mbalimbali za dunia katika mashindano hayo, suala ambalo linazidisha kiwango na ubora wake. 821408