IQNA

Chuo Kikuu cha Madina chafungua Taasisi ya Utafiti wa Qur'ani

22:22 - July 06, 2011
Habari ID: 2150263
Kwa msaada ya Wizara ya Elimu ya Juu ya Saudia, Taasisi ya Utafiti wa Qur'ani ya Noor imefunguliwa katika Chuo Kikuu cha Taybah katika Mji wa Madina.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Iqtisadia, taasisi hiyo imeanzishwa kwa lengo la kutumia teknolojia ya mawasiliano kuhudumia Qur'ani Tukufu na sayansi za Qur'ani ili kuwasaidia wanaotaka maelezo ya Qur'ani Tukufu.
Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Taybah katika mji wa Madina Mansur al Nuzhah amesema kuwa, 'tumeamua kufungua taasisi hii ili kuratibu tovuti za Kiislamu na Qur'ani na vilevile programu za kompyuta za Qur'ani za watoto'.
820518
captcha