IQNA

Hafla za mwezi wa Shaaban zaadhimishwa Zimbabwe

22:27 - July 06, 2011
Habari ID: 2150271
Idara ya Utamaduni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Zimbabwe imeandaa hafla kwa minasaba ya kuadhimisha kuzaliwa Imam Hussein AS, Imam Sajad AS na Hazrat Abbas AS.
Kwa mujibu wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO) lenye makao yake mjini Tehran, hafla hiyo itafanyika Julai 7 baada ya Sala za Magharibi na Isha katika Hoteli ya Wairani mjini Harare.
Kati ya watakaotoa hotuba katika kikao hicho ni Abu Khalili Naibu Mkuu wa Jamii ya Walebanoni nchini Zimbabwe na Bw. Asadi Muwahhed, Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Zimbabwe.
Mada za hotuba zitakuwa 'Kuzaliwa Imam Hussein AS kwa mtazamo wa Mtume Mtukufu SAW' na 'Historia ya minasaba ya Kiislamu kwa mujibu wa Qur'ani na Hadithi'.
820552
captcha