IQNA

Al Azhar kufungua kituo cha kutarjumi vitabu vya Kiislamu

22:29 - July 06, 2011
Habari ID: 2150272
Chuo Kikuu cha Al Azhar kimeafiki kufungua kituo cha kutarjumi vitabu vya Kiislamu kutoka lugha ya Kiarabu kwa lugha nyinginezo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Al Wafd, uamuzi huo umechukuliwa katika kikao kilichoongozwa na Ahmad Al Tayyeb Sheikh Mkuu wa Al Azhar. Katika kikao hicho Baraza Kuu la Al Azhar lilichunguza nafasi ya chuo hicho katika kusambaza fikra za mitazamo ya wastani za Kiislamu.
Mkutano huo uliofanyika mjini Cairo pia ulihudhuriwa na Abdul Hamid Abu Suleiman ambaye ni mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Fikra za Kiislamu.
Aidha baraza hilo limeamua kuondoa sharti la umri kwa wasio Waarabu wanaotaka kusoma Al Azhar.
820429
captcha