IQNA

Insaiklopidia ya Qur'ani na Haditi kuzinduliwa

22:31 - July 06, 2011
Habari ID: 2150283
Mjumuiko wa Mafundisho ya Qur'ani na Hadithi wenye anwani ya 'Insaiklopidia ya Qur'ani na Haditi' itazinduliwa mapema mwezi Oktoba nchini Iran.
Hujjatul Islam Sayyid Mohammad Kazem Tabatabai Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Sayansi za Hadithi mjini Tehran amesema mjumuiko huo ni matokeo ya utafiti wa miaka 19 uliofanywa na Taasisi ya Darul Hadith kuanzia mwaka 1992.
Amesema mjumuiko huo una juzuu 60 kwa lugha ya Kiarabu na juzuu 100 kwa Kiarabu-Kifarsi.
Mradio huo umetekelezwa chini ya usimamizi wa mwanazuoni mwandamizi wa Iran Ayatullah Reyshahri kwa ushirikiano na watafiti katika Taasisi ya Darul Hadith.
819848
captcha