IQNA

Mazungumzo baina ya dini mbalimbali hayana maana ya kuuanzishwa dini moja

16:28 - July 09, 2011
Habari ID: 2150295
Mkuu wa Baraza la Kipapa la Vatican amesema kuwa lengo la kuanzishwa mazungumzo kati ya dini mbalimbali ni kutayarisha uwanja mzuri wa maelewano na kuishi pamoja kwa amani kati ya wafuasi wa dini tofauti na si kuanzisha dini moja ya dunia nzima.
Kardinali Jean Louis Tauran amesema mazungumzo kati ya dini mbalimbali hayana maana ya viongozi wa dini tofauti kuketi pamoja na kuchukua uamuzi wa kuanzisha dini moja kwa ajili ya walimwengu wote bali mazungumzo hayo yanakusudia kutayarisha mazingira bora ya wafusi wa dini zote za Uislamu, Ukristo na Uyahidi kuishi pamoja kwa amani na utulivu.
Ameongeza kuwa wakati mwingine kunajitokeza ufahamu usiokuwa sahihi kwamba maana na mazungumzo kati ya dini tofauti ni kuchunguza hitilafu zilizopo kati ya dini tofauti na hata baadhi ya watu wanadhani kuwa viongozi wa dini mbalimbali wanataka kuanzisha dini moja kwa ajili ya walimwengu wote. Kardinali Jean Louis Tauran amesisitiza kuwa mazungumzo hayo hayafanani na mazungumzo ya kisiasa wala hayana lengo la kushusha chini dini moja na kuimarisha nyingine. 820260
captcha