IQNA

OIC yalaani vitongoji vya walowezi wa Kizayuni

10:17 - July 09, 2011
Habari ID: 2150756
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC Profesa Ekmeleddin Ihsanoglu amelaani vikali uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kujenga vitongoji 900 vipyahuko Quds Mashariki pamoja na vitongoji vingine 400 Ukingo wa Magharibi.
Taarifa ya OIC imesema kuendelea sera hizo za kichochezi za Utawala wa Kizayuni wa Israel ni ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa jambo ambalo linailazimu jamii ya kimataifa kuingilia kadhia hiyo.
Profesa Ihsanoglu ameitaka Kamati ya Pande Nne inayojumuisha Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Russia na Marekani kuchukua hatua za kuzuia ujenzi wa vitongoji hivyo vya Wazayuni na kuhakikisha Wapalestina wanarejeshewa haki zao.
821900
captcha