Kwa mujibu wa tovuti ya Al Wafd, kongamano hilo la siku mbili ni la kwanza la aina yake kuandaliwa na jumuiya hiyo mjini Cairo. Wanazuoni na watafiti wa Kiislamu kutoka maeneo yote ya dunia wanatazamiwa kuhudhuria.
Sheikh Fathi Abul Ward Mkurugenzi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu amesema mada zitakazochunguzwa katika kikao hicho ni pamoja na “Uislamu na Dini Nyinginezo”, “ Malengo ya Sheria za Kiislamu”, “Mazungumzo katika Uislamu” na “ Mazungumzo ya Kifiqhi Katika Uislamu”.
Aidha kongamano hilo litajadili mazungumzo ya Kiislamu kuhusu wanawake, maendeleo na suhula za kisasa.
821886