Hayo yamesemwa na Ismail al A'wani, mwakilishi wa Tunisia katika kitengo cha hifdhi ya Qur'ani cha Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani yaliyomalizika hivi karibuni mjini Tehran. Al A'wani mwenye umri wa miaka 20 ambaye amehifadhi Qur'ani nzima amesema: "Hii ni mara yangu ya kwanza kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Iran na kwa mtazamo wangu mashindano haya na kiwango cha washiriki ni cha juu sana kiasi kwamba ni vigumu mno kuweza kuchuana nao."
Msomaji huyo wa Qur'ani kutoka Tunisia amesifu maandalizi mazuri ya Mashindano ya 28 Kimataifa ya Qur'ani mjini Tehran na akasema amefurahia mno kukutana kwa karibu na Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Ameongeza kuwa ni jambo la kufurahisha mno kuona Rais wa nchi akihudhuria katika mashindano ya Qur'ani na kuketi na wapenzi wa kitabu hicho kitukufu.
Kuhusu jinsi alivyohifadhi Qur'ani nzima, Ismail al A'wani amesema: "Nilianza kuhifadhi Qur'ani nikiwa na umri wa miaka 17 na nimefanikia kuhifadhi kitabu hicho kitukufu katika kipindi cha miaka mitatu."
Amewausia vijana kusoma, kuhifadhi na kutekeleza mafundisho ya Qur'ani Tukufu. 821902