Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Wakfu nchini Misri Bw. Abdulqadir Sarhan, mashindano hayo yataendelea hadi 20 mwezi wa Ramadhani.
Amesema washiriki watashindana katika kuhifadhi Qur'ani kikamilifu kwa kuzingatia hukumu za Tajweed na kufasiri baadhi ya juzuu za Qur'ani Tukufu. Aidha kutakuwa na mashindano ya kuhifadhi Juzuu 20 na 10 za Qur'ani..
Mashindano hayo yanatazamiwa kuwa na washiriki 100 kutoka Misri na nchi nyinginezo duniani.
821864