IQNA

Mashindano ya taifa ya Qur'ani ya wanawake yamalizika Brunei

18:58 - July 10, 2011
Habari ID: 2152056
Mashindano ya kitaifa ya kiraa ya Qur'ani makhsusi kwa ajili ya wanawake nchini Brunei yalimalizika jana. Mashindano hayo yamefanyika kwa lengo la kuwaenzi wanawake wateule.
Mashindano hayo yamefanyika kwa hima ya Taasisi ya Uongofu ya wasichana wa Brunei katika vitengo viwili vya watoto wadogo na watu wazima katika shule ya Sayyiduna Hassan.
Washiriki katika mashindano hayo walikuwa katika vitengo kadhaa vya umri wa miaka 7 hadi 12, miaka 13 hadi 16, miaka 17 hadi 21, miaka 22 hadi 30.
Mashindano hayo ya Qur'ani ya wanawake wa Brunei ni sehemu ya harakati za Taasisi ya Uongofu ya wasichana wa nchi hiyo ambayo hufanyika kila mwaka tangu mwaka 1986.
Mashindano hayo yanafanyika kwa lengo la kuwahamasisha wanawake kusoma na kutadabari Qur'ani Tukufu na kutumia mafundisho ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu katika maisha yao ya kila siku. 822881

captcha