IQNA

Maandamano dhidi ya kufungwa kituo cha ibada cha Waislamu Ufaransa

23:19 - July 10, 2011
Habari ID: 2152096
Taasisi ya Kiilsamu ya al Houda ya Ufaransa imewataka Waislamu wa mji wa Gennevilliers kufanya maandamano Ijumaa ijayo kupiga kitendo cha kufungwa kituo cha ibada cha Waislamu wa mji huo.
Afisa wa msikiti wa al Houda katika mji huo amewataka Waislamu kuandamana Ijumaa ijayo mbele ya jengo la Meya wa Gennevilliers kama ishara ya kuonyesha malalamiko yao dhidi ya uamuzi wa Halmashauri ya mji huo wa kufunga kituo cha ibada cha Waislamu.
Awali Jumuiya ya al Houda ilimwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa ikieleleza malalamiko ya Waislamu dhidi ya kitendo hicho lakini wizara hiyo imepuuza malalamiko hayo.
Msikiti wa al Houda ulijengwa mwaka 1981 na una uwezo wa kupokea Waislamu 400 lakini meya wa mji wa Gennevilliers ameamua kufunga msikiti huo kwa kisingizio kwamba eneo hilo ni mali ya serikali. 822884



captcha