Shughuli hiyo inasimamiwa na Jumuiya ya al Furqan ya jimbo la Umm al Bawaqi nchini Algeria.
Shughuli za Wiki ya Kimataifa ya Mafunzo ya Qur’ani nchini Algeria zinahudhuriwa na mwakilishi wa Waziri wa Waqfu wa nchi hiyo, maulamaa, wahubiri wa Kiislamu, maimaamu wa misikiti na wananchi wa kawaida.
Mwakilishi wa Waziri wa Wakfu wa Algeria amesisitiza katika shughuli hizo ambazo zitaendelea kwa muda wa siku tatu juu ya udharura wa kulea kizazi kinachotambua thamani za Kiislamu na zinazooana na Qur’ani na Hadithi za Mtume (saw).
Afisa wa Jumuiya ya al Furqan pia alitoa ripoti kuhusu shughuli za jumuiya hiyo katika uwanja wa kutoa mafunzo ya Qur’ani Tukufu na kueneza thamani za dini ya Kiislamu kati ya vijana na matabaka mbalimbali ya wananchi. 822887