IQNA

Mashindano ya Qur'ani Malaysia kutangazwa moja kwa moja Iran

23:52 - July 11, 2011
Habari ID: 2152769
Mashindano ya 53 ya Qur'ani Tukufu ya Malaysia yatatangazwa moja kwa moja na Kanali ya Televisheni ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kwa mujibu wa idara ya habari ya Televisheni ya Qur'ani ya Iran, sehemu za mashindano hayo zitarushwa hewani moja kwa moja kutoka Malaysia kuanzia Julai 16 kila siku kwa wiki moja kuanzia saa kumi hadi saa moja kwa majira ya Tehran.
Mshindi wa pili katika mashindano ya kitaifa ya Qur'ani ya Shirika la Awqaf la Iran atawakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashindano hayo ya Qur'ani ya Malaysia.
Sehemu ya sherehe za ufunguzi na kufunga mashindano hayo zitatangazwa moja kwa moja na Televisheni ya Qur'ani.
822943








captcha