Kwa mujibu wa jarida la intaneti la 'Islamic Arts Magazine', mashindano hayo ambayo kwa Kiingereza yanajulikana kama 'Silk Rout StyleIn Jilbab Design 2011 Competition' yataanza tarehe 23 Julai na kumalizika Agosti 21.
Wanaotaka kushiriki wanaweza kutuma michoro yao kabla ya tarehe hiyo. Tarehe 14 Septemba mchoro 20 bora itafikishwa mbele ya jopo la majaji na baada ya wiki moja mchoro bora zaidi utachaguliwa na jina la mshindi litatangazwa Septemba 24.
Mchoro bora utashonwa, kutayarishwa na kuzinduliwa katika Tamasha ya Nguo za Msimu wa Machipuo Mwaka 2012 la Shirika la Nguo za Kiislamu la 'Silk Rout'.
Mbali na kupokea zawadi ya Paundi 500 za Uingereza, mshindo atapata fursa ya kupata mafunzo ya wiki sita yatakayotolewa na jopo la wachoraji mitindo katika Shirika la Nguo za Kiislamu la 'Silk Rout'.
823747