Mnara huo una vipaza sauti vikubwa ambavyo vitakuwa na uwezo wa kufikisha sauti ya adhana umbali wa kilomita saba. Aidha mnara huo una mataa 21,000 ambayo mwangaza wake utaweza kumulika eneo la umbali wa kilomita 30.
Gazeti la Kiarabu la Saudia Okaz, limeandika kuwa mnara huo umetengenezwa kwa dhahabu tupu lakini halikutaja ukubwa wake.
Mnara wa Saa katika mji mtakatifu wa Makka una urefu wa mita 601 na unashabihiana na ule Mnara wa Big Ben wa London.
Wataalamu wengi wa masuala ya historia ya Uislamu duniani wamekosoa ujenzi wa mnara huo ambao umeiga usanifu majengo wa Ulaya na hivyo kuharibu mandhari ya kihistoria ya al Ka'aba Tukufu.
823133