Mkuu wa kitengo cha falaki katika maonyesho hayo Hujjatul Islam Mohammad Taghdiri amesema maonyesho hayo yatajumuisha mada kama vile mwezi mwandamo, muelekeo wa kibla na kutizama nyota usiku.
Ameongeza kuwa kitengo hicho cha falaki kitasimamiwa na taasisi ya nujumi ya Haram ya Abdul Azim Hassani AS mjini Tehran .
Nujumi kwa watoto, kalenda ya Kiislamu, nyakati za sala za maeneo mbalimbali ya dunia ni kati ya programu za kitengo hicho.
Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yatafanyika katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
824296