IQNA

Washindi wa mashindano ya Qur'ani Uganda waenziwa

14:28 - July 12, 2011
Habari ID: 2153305
Washindi wa mashindano ya Qur'ani ya Al Maher nchini Uganda wametunukiwa zawadi Julai 11 katika mji mkuu wa nchi hiyo Kampala.
Mashindano hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani kwa ushirikiano na Kituo cha Kuhifadhi Qur'ani cha Ubay bin Ka'ab cha Uganda.
Wanafunzi 50 wa kike na kiume walishiriki katika mashindano hayo katika vitengo vya kuhifadhi Qur'ani kamili, juzuu 25, juzuu 15 na Hadithi.
Jopo la majaji lilijumuisha wataalamu 6 wa Qur'ani kutoka Uganda, Sudan, Misri, mwakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani na mashirika kadhaa ya Kiislamu.
Wazungumzaji katika hafla hiyo wamepongeza juhudi za Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani na kutoa wito kwa vijana Waislamu wafanya bidii kuhifadhi Qur'ani na kutekeleza mafundisho yake.
824411
captcha