IQNA

Kongamano la kimataifa la "Uislamu Barani Afrika" kufanyika Malaysia

14:20 - July 12, 2011
Habari ID: 2153319
Kongamano la kimataifa la "Uislamu Barani Afrika: Mirengo ya Kifikra, Vyanzo vya Kihistoria na Mipango ya Utafiti" litafanyika kuanzia tarehe 19 hadi 21 Julai katika mji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur.
Kongamano hilo litasimamiwa na Jumuiya ya Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu (FUMI) kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Malaysia.
Miongoni ma mambo yatakayojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na 'Mbinu za Kulingania na Kueneza Uislamu Barani Afrika', 'Wahajiri wa Kisiasa na Mchango wao katika Kueneza Uislamu Afrika' na 'Uislamu na Waislamu Barani Afrika: Uchunguzi wa Kivitendo'.
Masuala mengine yatakayojadiliwa ni kuhusu utamaduni na turathi za Kiislamu Afrika, uhusiano wa kilugha katika nchi za Kiarabu za Afrika, nakana zilizoandikwa kwa lugha ya Kiarabu barani Afrika na vyanzo vya Kiislamu na Kiarabu vya historia ya Afrika.
Mkutano huo ambao utahudhuriwa na wasomi kutoka vyuo vikuu vya ulimwengu wa Kiislamu utatazama upya mipango ya sasa ya kustawisha utamaduni wa mazungumzo kati ya Uislamu na Ukristo na pia njia bora na za kisasa zaidi za kukuza uhusiano wa Waislamu na Wakristo barani Afrika. 824266
captcha