IQNA

Msahafu wa kitaifa kuzinduliwa Mauritania

14:56 - July 12, 2011
Habari ID: 2153355
Msahafu wa kitaifa wa Mauritania ulipewa jina la Shanqit utazinduliwa rasmi kufikia mwishoni mwaka huu wa 2011.
Shirika rasmi la habari la Mauritania (AMI) limeripoti kuwa uchapishaji wa msahafu wa kitaifa umeanza kwa amri ya Rais wa nchi hiyo.
Msahafu wa kitaifa wa Mauritania unaandikwa kwa hati rasmi za nchi hiyo kwa mujibu wa riwaya ya Warsh kutoka kwa Nafi.
Waziri wa Masuala ya Kiislamu na Elimu wa Mauritania Ahmad Ould al Nini jana alikagua kazi ya uchapishaji wa msahafu huo wa kitaifa katika kamati maalumu ya kuchunguza uchapishaji na usahihishaji wa msahafu huo mjini Nouakchott. Vilevile alitembelea kiwanda cha uchapishaji cha al Nur kinachochapisha msahafu huo wa kitaifa wa Mauritania.
al Nini pia ameitaka kamati maalumu inayosimia kazi hiyo kuhakikisha kwamba unachapishwa kabla ya kumalizika mwaka huu wa 2011.
824520

captcha