Shirika la habari la IINA limeripoti kuwa mahfali hiyo itahudhuriwa na idadi kubwa ya wanavunzi Waislamu wa vyuo vikuu na wanachama wa Jumuiya ya Vijana Waislamu, Taasisi ya Kiislamu ya Sadr na Jumuiya ya Kiislamu ya Anna Catherina ya Guyana.
Mahfali hiyo itakamilisha kazi zake kwa kuarifisha mashairi na qasida bora za kumsifu Mtume Muhammad (saw).
Mahfali ya qasida za kumsifu Mtume Mtukufu ilifanywa kwa mara ya kwanza na Taasisi ya Kiislamu ya Sadr ya Guyana. Duru ya saba ya mahfali ya kimataifa ya kumsifu Mtume ilifanyika mwaka jana huko Trinidad na Tobago na duru ijayo itafanyika nchini Guyana. 824624