Kwa mujibu wa gazeti la Al Anba, mashindano hayo yatakuwa na vitengo vya Tajweed na Hifdhi na mwaka huu kaulimbiu ya mashindano hayo itakuwa 'Qur'ani yangu Imeniongoza'.
Abdul-Mohsen Al-Kharafi kutoka Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kiislamu amesisitiza kuwa mashindano ya Qur'ani yana nafasi muhimu katika kulea kizazi cha mahufadhi na maqarii wenye umahiri ambao wanaweza kuiwakilisha Kuwait katika mashindano ya kimataifa.
Aidha ametoa wito kwa washiriki kutumia fursa ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kujiimarisha kwa ajili ya mashindano.
Msikiti Mkuu wa Kuwat utakua mwenyeji wa mashindano hayo.
Washiriki pia wametakiwa kupata kijitabu cha hukumu za Tajweed kupitia tovuti ya www.awqaf.org/quran au taasisi zinazoshiriki katika uandilizi wa mashindano.
824327