Heidar Moslehi, Waziri wa Usalama wa Taifa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taifa la Iran liko tayari kukabiliana vilivyo na njama zozote za maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu hususan Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Akizungumza kabla ya hotuba za sala ya Ijumaa ya jana mjini Tehran, Moslehi alisema kuwa, maadui wa taifa hili la Kiislamu wamekuwa wakipanga na kupangua kila uchao njama za kuihujumu Iran katika nyanja zake zote ikiwemo ya utamaduni, jamii na uchumi.
Waziri wa Usalama wa Taifa wa Iran amesisitiza kuwa,Tehran inaendelea kupambana vilivyo na vita laini vinavyondeshwa na maadui wa Uislamu dhidi ya taifa hili kwa miongo kadhaa sasa maadui ambao lengo lao kuu ni kutaka kuvunja Mapinduzi ya Kiislamu.
Waziri Moslehi ameongeza kuwa, Wizara ya Usalama wa Taifa ya Iran si tu imekuwa ikifuatilia masuala ya usalama wa wananchi wake lakini pia imekuwa ikifuatilia kwa karibu na kukusanya data na taarifa za kiintelijensia ili kuzima njama zote za maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
826110