IQNA

Conakry, Mji Mkuu wa Kiutamaduni wa Ulimwengu wa Kiislamu

16:56 - July 18, 2011
Habari ID: 2155938
Sherehe za kuadhimisha kuteuliwa mji wa Conakry kama mji mkuu wa kiutamaduni wa Ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2011 zimefanyika Julai 18.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA kitengo cha Afrika, wawakilishi wa taasisi za kimataifa za Kiislamu pamoja na viongozi wa kidini na kisiasa wa Jamhuri ya Guinea Conakry wameshiriki.
Mji wa Conakry ulitangazwa na Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni ISESCO kuwa mji mkuu wa Kiislamu mwaka 2011 kwa eneo la Afrika.
Mustafa Ahmad Ali Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu amewakilisha ISESCO katika hafla hiyo.
Mwaka 2005 Mji Mtakatifu wa Makka ulitangazwa kama Mji Mkuu wa Ulimwengu wa Kiislamu. Tokea wakati huo, kila mwaka ISESCO hutangaza miji mitatu Afrika, Asia na Ulimwengu wa Kiarabu kuwa miji mikuu ya kiutamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu kila mwaka.
826635
captcha