Taarifa iliyotolewa na Baraza la Maimamu wa Jamaa wa Luxembourg imesema kuwa mwezi mtukufu wa Ramadhani utaanza tarehe 1 Agosti na kumalizika tarehe 29 ya mwezi huo.
Imesisitiza imetangaza uamuzi huo kwa kutilia maanani mahesabu ya kisayansi na amri ya Baraza la Ulaya la Fatuwa na Uchunguzi wa Kiislamu ya udharura wa umoja na mshikamano katika kuainisha nyakati za sikukuu za Kiislamu.
Taarifa hiyo ya Baraza la Maimamu wa Jamaa wa Luxembourg imeongeza kuwa tarehe 31 Julai litatangaza rasmi kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani. 827170