IQNA

IQNA kuandaa kikao cha “Msikiti na Tafsiri ya Qur’ani”

13:13 - July 19, 2011
Habari ID: 2156347
Shirika la Habari za Qur’ani la Kimataifa IQNA lenye makao yake nchini Iran limeandaa warsha itakayojadili maudhui ya “Msikiti na Tafsiri ya Qur’ani”. Warsha hiyo itafanyika Julai 20 katika makao makuu ya IQNA mjini Tehran.
Kikao hicho kitahudhuriwa na Hujjatul Islam Hamid Mohammadi Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran anayeshughulikia masuala ya Qur’ani kati ya wataalamu wengine.
Kikao hicho kitakuwa cha mwisho katika mfululizo wa vikao vinavyochunguza nafasi ya misikiti katika kustawisha utamaduni wa Qur’ani nchini Iran.
Washiriki watajadili nafasi ya tafsiri ya Qur’ani katika misikiti.
Vikao vya huko nyuma kati ya mengine vilijadili mipango kadhaa ya kustawisha utamaduni wa Qur’ani miongoni mwa vijana katika misikiti nchini.

826982
captcha