Aidha wametilia mkazo suala la kuweko ushirikiano zaidi wa pande mbili kwa ajili ya kupambana na janga hilo.
Mwandishi wa Redio Tehran amemnukuu Rais Ahmadinejad akisema katika mazungumzo ya simu aliyofanya jana na Rais Hamid Karzai wa Afghanistan kuwa, wananchi na serikali ya Iran wamesikitishwa sana na mauaji ya kigaidi yaliyofanywa dhidi ya ndugu wa kiume wa Rais Karzai huko kusini mwa Afghanistan na kuongeza kuwa, kuna haja ya kushirikiana zaidi pande mbili katika kupambana na magaidi.
Rais Ahmadinejad aidha amesema kwamba, maadui kamwe hawajawahi kuwa na nia ya kuleta amani na maendeleo kwa Afghanistan wala kwa taifa jingine lolote, bali siku zote wanafanya njama za kuvuruga hali ya usalama katika nchi za eneo hili ili wapate kisingizio cha kufanikisha malengo yao haramu.
Kwa upande wake, Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amewashukuru wananchi na serikali ya Iran kwa kuwa pamoja na taifa la Afghanistan katika msiba huo na kusema kuwa, taifa kubwa la Iran siku zote liko pamoja na ndugu zao Waafghani.
Aidha ameelezea matumaini yake ya kuendelezwa misaada ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika juhudi za kudumisha amani na maisha ya heshima kwa wananchi wa Afghanistan.
827594