Mashindano hayo ya hifdhi na tarteel yanafanyika kwa himaya ya Taasisi ya Darul Qur’ani ya Imam Ali bin Abi Twalib AS.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo ya siku tatu yatakuwa na vitengo viwili vya walio chini ya umri wa miaka 16 na walio juu ya umri wa miaka 16 katika Ukumbi wa Husseiniya Fatimiyun. Mashindano hayo yatajumuisha hifdhi ya juzuu moja, juzuu tano, juzuu 10, juzuu 20 na Qur’ani kamili.
Hadi sasa watu 700 wamejisajili kushiriki katika mashindano hayo.
827361