IQNA

IQNA yaanzisha kitengo cha wenye ulemavu wa macho

15:25 - July 19, 2011
Habari ID: 2156395
Shirika la Habari za Qur’ani la Kimataifa IQNA lenye makao yake nchini Iran leo Julai 19 limezindua kitengo cha walio na ulemavu wa macho.
Hafla hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya IQNA mjini Tehran imehudhuriwa na Ali Reza Zojaji mkuu wa masuala ya utamaduni katika Shirika la Jihadi ya Vyuo Vikuu Iran , Hujjatul Islam Taghavi Mkuu wa Shirila la Wanachuo wa Iran la Harakati za Qur’ani na Mkuu wa Idhaa ya Qur’ani ya Iran kati ya maafisa wengine wanaohusika na harakati za Qur’ani nchini.
Hafla hiyo ilianza kwa kusomwa aya za Qur’ani Tukufu na kufuatiwa na hotuba za maafisa waliohudhuria. Hujjatul Islam Taghavi amesema kuanziwa kitengo cha wenye ulemavu wa macho ni hatua muhimu na ya aina yake amabayo inaashiria uzingatiwaji thamani za mwanadamu.
Aidha katika hafla hiyo jarida la Sepideh Afarin la watu wenye ulemavu wa macho limezinduliwa
827742
captcha