Warsha hiyo na mafunzo iliyoanza tarehe 4 Julai inajadili mchango wa dini mbalimbali kama wenzo muhimu kwa ajili ya kuimarisha amani ya kimataifa.
Wasimamizi wa warsha hiyo wanafanya juhudi za kuwaeleza wanafunzi wa vyuo vikuu mchango na nafasi ya dini katika kueneza amani na utulivu kote duniani na kuwayatarisha kwa ajili ya kutoa mchango katika medani hiyo kama wawakilishi wa mazungumzo kati ya dini mbalimbali.
Warsha hiyo ya mafunzo itakayoendelea hadi tarehe 8 Agosti inasimamiwa na Jumuiya ya Mazungumzo kati ya Dini Mbalimbali ya Uswisi kwa ushirikiano wa Taasisi ya Kiislamu ya Taaruf na Jumuiya ya Kikristo ya Kanisa la Uswisi. 827618