Kwa mujibu wa Idara ya Habari ya Taasisi ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu, Ayatullah Muhammad Ali Taskhiri amemshukuru Sheikh Ahmad al Tayyeb kwa hotuba yake ya hivi karibuni ambapo alitaka kuhuishwa utamaduni wa kukurubisha madhehebu ya Kiislamu na ustawishwaji wa kina wa uhusiano baina ya madhehebu za Kiislamu.
Ayatullah Taskhiri amemkaribisha al Tayyeb kutembelea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Amemuomba Mwenyezi Mungu ampe taufiki Sheikh wa Al Azhar katika kufikia malengo ya Al Azhar ambayo ni kulinda mafanikioa ya umma wa Kiislamu.
Hivi karibuni Ahmad al Tayyib Shekhe Mkuu wa Al Azhar alipinga hujuma ya propaganda dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia inayoenezwa na baadhi ya makundi yenye misimamo mikali. Aidha alikosoa kanali za televisheni za satalaiti ambazo zinawavunjia heshima Mashia. Sheikh Ahmad Tayyib alisema: “Mashia ni sehemu isiyotenganika ya umma wa Kiislamu. Mashia na Masuni wanahitilafia tu katika baadhi ya masuala ya pembeni”.
Aidha hivi karibuni Shekhe wa al Azhar alitangaza kuwa tayari Chuo Kikuu cha Al Azhar nchini Misri kuwapokea wanafunzi wa Kishia na kuwaruhusu Marajii na maulamaa wakubwa wa Kishia kujiunga na Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya Al Azhar.
827486