Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Abdullah bin Abdul Muhsin al Turki amesema umma wa Kiislamu unakabiliwa na changamoto kubwa na baadhi ya nchi za Kiislamu zimetumbulkia katika hali ambayo inapaswa kuchunguzwa na kujadiliwa.
al Turki amesema hali hiyo mbaya ya nchi za Kiislamu ina sababu zake ambazo zinapaswa kutafutiwa ufumbuzi kwa mujibu wa mafundisho sahihi na halisi ya Uislamu.
Ameongeza kuwa Jumuiya ya Ulimwengu wa Kiislamu imewaalika wasomi na maulamaa wa Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali duniani kwa lengo la luchunguza hali ya sasa ya umma wa Kiislamu, matatizo yaliyopo na ufumbuzi wake.
Ameawma kwamba mkutano huo utadili masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na ujahili kuhusu hakika ya Uislamu, hitilafu na njama za maadui za kuzusha mifarakano kati ya Waislamu, hali ya kiuchumi na kijamii ya nchi za Kiislamu, wajibu wa serikali na wananchi na uratibu wa juhudi za serikali na wananchi katika kupambana na migogoro mbalimbali. 829703