IQNA

Semina ya Elimu ya Juu ya Kiislamu na Changamoto za Sasa kufanyika Japan

9:34 - July 25, 2011
Habari ID: 2159332
Semina ya kimataifa ya 'Marekebisho ya Elimu ya Juu ya Kiislamu katika Kukabiliana na Changamoto za Sasa' imepangwa kufanyika tarehe 30 na 31 Julai katika mji wa Nagoya nchini Japan.
Semina hiyo itasimamiwa na Chuo Kikuu cha Nagoya, Chuo cha Mafunzo na Ustawi wa Kibinadamu na Jumuiya ya Maendeleo ya Sayansi ya Japan.
Semina hiyo itachunguza elimu ya juu ya Kiislamu na uwano kati ya sayansi na dini, suala la kuhuishwa matukufu katika elimu za sasa, ustawi wa nguvu kazi, uhuru wa kielimu na kisayansi, haki za binadamu na Waislamu waliowachache au wengi katika jamii ya kiseculari.
Semina hiyo itahudhuriwa na wahadhiri na wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka maeneo mbalimbali. 830008


captcha